Catherine Jumanne amekuwa mwanamke wa kwanza kuendesha mabasi ya mwendo kasi jijini Dar es Salaam. Safari ya Catherine ilianzia jijini Arusha ambapo mara baada ya kupata taarifa ya taasisi ya WOW alituma maombi na kujiunga moja kwa moja Dar es Salaam.

Ndoto ya Catherine katika kupiga hatua kwenye maisha yake kupitia sekta ya usafirishaji ilitimia mara baada ya kumaliza mafunzo katika taassi ya WOW ambapo aliweza kupata ajira katika kampuni ya DART inayoendesha usafirishaji wa mabasi ya mwendo kasi.

– Women on Wheel Africa ni mpango maalimu wa kumkomboa mwanamke kiuchumi kupitia sekta ya Usafirishaji –

Dereva wa Mwendokasi wa Kike DSM